Kuna baadhi ya fursa zimeachwa kwa aji- li ya wafanya biashara wakubwa na hasa viwanda vya nje ikiwemo hii ya kushona mabegi ya safari.

Inawezekana ni sababu ya fikra tu kuwa lazima uwe na mtaji mkubwa na utaalam mkubwa kushona mabegi makubwa ya sa- fari.

Angalia begi lako moja la safari la kitam- baa au ngozi, achana na ya plastic na uone kama lina maajabu yoyote, na utagundua halina chochote cha ajabu ambacho haki- wezi kushonwa na mtu mwenye cherehani yake aliyejibanza kibarazani.

Tofauti kati ya pochi au mikoba midogo ya wadada na mabegi ya safari ni ukubwa tu. Kwa mfano kushona begi la safari unaweza kutumia mita moja ya Ngozi, au PVC au Ki- tambaa wakati mita moja hiyo unaweza

kutoa vipochi vidogo vinne.

Kwa maana hiyo, kama una cherehani ta- yari basi ukiwa na Shilingi 15,000 unawe- za kushona mabegi hata ma 3 mpaka ma 3 ya safari.

Utaalam ni uleule na material ni yaleyale na vifaa ni vilevile kama vya mikoba midogo ya wadada. Ukiwa fundi mzuri na makini hasa kwenye kushona mikanda ya mabegi basi unaweza hata kuweka lebo za brand kubwa na ukipeleka kwa wauzaji wa mage- gi hamna atakaye kushtukia.

Ukiwa mvumilivu basi unaweza kutoa kwa lebo yako ambapo itakuchukua miaka kad- haa kujenga jina na kukubalika na baada ya hapo utafanya kazi kwa faida.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *