Pamoja na kuwa wachaga na wapiga shoe shine wanaweza kushona viatu kuanzia asilimia sifuri mpaka 100 bila kutumia mashine yoyote wala umeme bado watu wengi walidhani kushona viatu ni kazi ya kimaskini.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mwamko wa watu kufungua viwanda vidogo vya viatu na wewe unaweza kuwa ni mmoja wapo kwani mahitaji yake yanaweza kuwa sio makubwa kama unavyodhani.

Unaweza kujikita katika kushona viatu, vi- kiwemo vya shule pamoja na vya kawaida tu, vifaa vya muhimu ni kama vya kukatia Ngozi ambapo kama una mtaji basi unanunua mashine inaitwa click mashine ya kukatia Ngozi, pamoja na die zake lak- ini kama huna unakata Ngozi kwa kisu tu kwa kutumia pattern za box badala ya die.

ukimaliza kukata unaenda steji ya kuunganisha vipande mbalimbali vya Ngozi ulivyokata kwa kutumia cherehani kubwa za industrial zipo zinauzwa kariakoo lakini hata mashine ndogo zinazotumia sindano kubwa kuweza kupenya ngozi zinaweza kufanya kazi hii. Mashine hizi za cherehani  zinapatikana kwa wingi sana zikiwa mpya na used.

Ukishaunganisha vipande kwa cherehani unavivisha kwenye “lasts” amabayo ni maplastiki magumu yenye shape ya mguu wa mtu, utahitaji hizi last kwa kila size ya mguu na zinapatikana kwa Woisso salasala au kariakoo.

Ukisha visha last unafanya mchakato unaitwa lasting ambao ni kama unakandamizia kwenye last vipande vya ngozi ya viatu ulivyoviunganisha ili ngozi ipate shape ya kiatu pamoja na kuunganisha ile soli laini ya kati ambayo ni ya box maalum au in- sole, yani soli ya ndani. Unatumia nyundo na vimisumari vidogo vya viatu hapa. Laki- ni mashine zake zipo…kuanzia dola 15,000 katika mji wa Foshani China. Naweza kuk- upeleka ukinilipia nauli.

Ukimaliza mchakato wa lasting ambapo unaunganisha insole na ngozi basi mchaka- to unaofuatia ni wa kuweka Soli.

kabla hujaweka soli inabidi uipake soli gundi ya moto halafu uiweke soli kwenye oven maalum ipate moto kiasi , unaiacha ipoe kidogo halafu ndio unaingusha soli na kiatu, ukimaliza kama una soling mashine unaitumia hiyo kukandamizia soli kwenye kiatu ili vigandamane, kwa haraka haraka mchakato wa kutengeneza kiatu utakuwa umekamilika.

Kama haujauogopa huo mchakato kwa sababu ni “labor na imput intensive” basi biashara hii itakufaa. Mchakato uliopewa hapa sio wa kusoma mtandaoni au kwenye vitabu, ni mchakato uliotoka kwa mmiliki wa kiwanda kidogo cha viatu..ambae pia ndio mwandishi wa hiki kitabu.

Vifaa vya msingi kwa kiwanda kidogo ni pamoja na

  • Cherehani
  • Visu vya kukatia ngozi au click machine
  • Die
  • Oven
  • Lasts
  • Soling mashine (ya kukandamizia kiatu kwenye soli)
  • Skive Machine kwa ajili ya kupunguza unene wa soli ili sindano iweze kupenya.

Material ya Kila siku ni pamoja na

  • Ngozi, PVC au Vitambaa
  • Gundi
  • Uzi
  • Sindano
  • Soli ya Ndani
  • Soli Ya Nje
  • Patterns

Biashara hii ni labour na capita intensive kwa maana inahitaji nguvu kazi ya watu kadhaa pamoja mtaji wa kutosha kuiendesha kwa angalau mwaka mmoja mpaka miwili kabla haijaweza kujitegemea.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *