Kama ni mtu wa IT, au hata sio wa IT, yani ulipata sifuri mbili kabisa zenye masikio katika hesabu unaweza kuanzisha biasha ya Website Designing kiurahisi kabisa, ili mradi unajua tu ni namna gani utapata wateja wa kuwatengenezea websites au Tovuti huku kwenye kutengeneza website ni kazi ndogo sana.
Hakikisha una Computer yenye mtandao tu.
Kukupa mwanga website designing unaweza kujifunza mwenyewe kupitia You Tube au ukanunua course za mtandaoni za shilingi 20,000 na ndani ya siku chache ukajua kila kitu kuhusu Website designing.
Unaweza kununua kozi za mtandaoni kutokea tovuti ya cousera na wapo waswahili wanafundisha kwa kiswahili pia. Hauna haja ya kujifunza mambo mazito ya IT kama HTML, CSS, JavaScript na mambo hayo ya ya ki IT yanayohusisha coding au programming. Wewe Jifunze Designing tu ambayo kimsingi utapitia mchakato ufuatao:-
Kwanza;-Nunua Domain kwanza, Google kuwapata wauzaji
Pili;-Lipia Hosting, atakae kuuzia domain anaweza kukuuzia na hosting pia.
Tatu:-Ukisha lipia watakutumia email yenye link itakayokupeleka eneo linatwa control panel
Nne;- na humo utafanya kujazajaza vitu vichache vya kuunganisha email zifanane na jina la tovuti, na ku customize mambo machache tu unayoyataka katika tovuti yako,
Tano:- Install WordPress utakauoikuta humo kwenye Control panel na itakuongoza kukupeleka kwenye dash board
Sita:- Utapata link za kutengeneza website yako kwa install template na ku customize plug ins kadhaa.
Ni rahisi sana hata mtoto wa darasa la 6 anaejielewa anaweza kufanya huu mchakato. Baada ya hapo unapost tu unachotaka kionekane kwenye website yako. Kupitia eneo limeandikwa “posts” kama blog kama hii unayosoma au tumia mahali pameandikwa pages kama sio blog na ni website ya kawaida. . Ni rahisi sana kivitendo kuliko haya maelekezo
Ищите в гугле