Mojawapo ya biashara zinazofanywa na GIF ni biashara ya kashata. Biashara hizi tunazipika kusifungasha na kuzisambaza katika masoko na ma supermarket. Biashara hii ilianza kidogo kidogo kwa kutengeneza kashata kidogo tu kwa ajili ya kula wenyewe nyumbani lakini baada ya kunogewa nkashauriwa mambo matamu namna hii usile mwenyewe. Vizuri kula na wenzio.
Nikaupokea ushauri huu na sasa hivi zinasambazwa katika mikoa mingi hapa Tanzania.
Pamoja na kuwa tulianza kidogo kidogo lakini hatukufanya kitu ambacho kiutaalam kinaitwa pilot study. Pilot ni kama kuijaribisha bidhaa sokoni kwanza kabla hujaamua kujilipua mzima mzima. Kwa mfano, mathalani, umeenda Mbeya ugenini halafu ukatengewa maji ya moto ya kuoga kwenye ndoo lazima uya test na vidole kwanza kabla hujajimwagia usije ukababuka ka,a mi ya moto sana au ukapata hyperthermia kama ni ya baridi sana. Kule ku test na mkono wako kama yana joto unalotaka ndio pilot study yenyewe.
Lakini pamoja na kuwa hatukufanya pilot study hatukuwa na kitu kingine kinaitwa MVP yaani Minimum Viable Product. Hii MVP ni bidhaa yenyewe unayotaka kuiingiza sokoni lakini kwanza unaitengeneza kwa gharama kidogo sana kwa ajili ya kuijalibisha sokoni. Yani Minimum kwenye MVP ipewe uzito hapo. Usiingiie gharama nyingi sana kununua mashine, malighafi nyingi, kuajiri wataalam, kupanga majengo ya gharama nakadhalika kabla ya kuijaribisha bidhaa sokoni uone kama itafanikiwa au haitafanikiwa.
Sasa kwe upande wa kashata kwa sababu hatukufanya mchakato wa MVP tukakutana na changamoto nyingi sana ambazo tunaendelea kupambana nazo mpaka leo.
Moja ya mfano ni baadhi ya malighafi tunazotumia kumbe hazizalishwi ndani ya nchi na watu wanaozileta huleta wakijisikia wao. Supply ikikata kwao na wewe hufanyi kazi, unaweza kufunga biashara au inakulazimu kwenda nje ya nchi. Ukisema uagize wewe mwenyewe china kiwandani unaambiwa kuna minimum order quantity na huko..kwamba lazima uchukua kilo au PC nyingi sana. Lakini MVP itakusaidia kujua kama kuna soko, muda wa maisha wa bidhaa katika shelf, muda wa kufundisha wafanyakazi, ushindani uliopo, ujazo na mambo mengine mengi sana,
Kwa mfano wa ukweli, kashata zetu tunatumia vifungashion ambvyo vina nakshi ya gold kwa ndani. Kumbe vifungashio hivyo supplier mkubwa ni mmoja tu nchi nzima. Akiishiwa huyu ndio basi tena na mtu unakuwa usha ji brand kuwa kashara za GIF zina muonekano huu. Ukibadilisha mwonekano unakuwa mgeni tena machoni kwa wateja. Kama tungekuwa na MVP halafu tukaiweka sokoni kwa hata miezi mitatu kwanza tungejua mapema kuwa Vifungashio ni tatizo.
Kwa hiyo usishangae kuona watu watu wengi wanawekeza sana, kwa gharama nyingi halafu biashara zao zinakufa haraka. Takwimu zinaonyesha asilimia 90 ya biashara mpya hufa ndani ya miaka 10. Watu wengi kodi yao ya mwaka wa kwanza ikiisha na wao wanafunga na kubadilisha biashara au wanakata tamaa kabisa sababu hawakujaribisha bidhaa sokoni kwanza kuangalia mwitikio wa soko na kuendelea kufanya mabadiliko kidogo kidogo huku wakikua. Unakuta mtu amewekeza kwenye saluni kwa sababu tu ameiona saluni fulani mahali inafanya vizuri, akaamua kuiga na wewe kufungua saluni ukiwa hujawahi kabisa kuifanya biashara hiyo huko nyuma na huna hata rafuki ambaye alishawahi kuifanya kwa miaka mingi akafanikiwa ili akushike mkono. Ukaenda kukodi frame kwenye jengo la ghorofa na kuweka Ma TV makubwa kila kona, unaweka ma sofa ya kusubiria, unaweka viti vya kunyolea vya mamilioni, unaweka vioo vya kutokea china vina TV humohumo, unalipa kodi milioni unusu kwa mwezi pamoja na malighafi za gharama, unatumia milioni 50. Baada ya sherehe ya uzinduzi unakuwa unapata mteja mmoja au wawili kwa siku ambazo zinatumika kununua Luku. Mwisho wa siku unakuwa umeingia hasara ya shilingi milioni 50. Ulitakiwa uanze na milioni 5 tu na kuboreka mdopgo mdogo.
Kwa ushauri wa biashara kwa wanaotaka kuanza na mambo kama haya tuwasiliane 0699354779.
Поиск в гугле