Nilishawahi kufungua biashara ya banda la chips Sinza Kijiweni, eneo lililochangamka kabisa na nilikuwa na chips nzuri na wateja walikuwa ni wengi wa kutosha. Lakini wateja wale walikuwa tayari kununua sahani ya chips kwa shilingi 2,500/-. Kusudi nipate faida kwa bei hiyo ilikuwa ni lazima kwa siku niuze angalau magunia manne ya chips, kila siku na mimi uwezo wangu ulikuwa ni kuuza gunia mbili tu kwa siku. Sikuona faida na baada ya mwaka mmoja nikafunga. Nilikuwa nahitaji kupata wateja watakaonunua Sahani moja angalau kwa kuanzia shilingi 3,000/- na kuendelea lakini nikashindwa kuwapata.
Leo tunajadili ujuzi ambao kila mfanyabiashara anaehitaji mafanikio kibiashara lazima awe nao. Bila ya kuwa na huu ujuzi biashara yoyote utakayo anzisha itabaki ama inzuga zuga kwa muda mrefu sana kabla ya kufa au ikafa mapema na ikifanikiwa basi itabaki kuwa ndogo tu.
Kuwa na bidhaa nzuri na yenye ubora sio siri ya mafanikio kibiashara, kuwa na location nzuri au bei ndogo sio siri ya mafanikio kibiashara, kuwa na huduma nzuri pamoja pamoja na watumishi wanaovaa uniform havimaanishi utafanikiwa. Kuwa na frame kwenye mall au mjengo mkubwa wa ghorofa sio guarantee ya mafanikio. Vyote hivi vilivyotajwa ni muhimu lakini sio msingi imara wa mafanikio kibiashara na kila siku tunashuhudia biashara zenye sifa hizo zikifungwa.
Unaweza ukafungua hospitali yako, ikaokoa maisha ya watu lakini wagonjwa, ambao ndio wateja wako usiwaone na ukafunga hospitali na sababu sio kwamba mwanzilishi ni daktari mbaya, anatoa huduma mbovu au ana majengo mabaya.
Mimi ni mmojawapo ya watu walionzisha na kufunga biashara nyingi sana, karibu kila biashara za Kiswahili unazozijua wewe nimejaribisha na kila mara nilipofunga biashara sababu kubwa ilikuwa ni kukosa wateja hasa wale unaowalenga na hivyo naweza kukuambia kwa kujiamini kabisa sababu kubwa biashara nyingi zinafungwa ni kwa ajiri ya kukosa wateja hasa wale ambao wapo tayari kununua bidhaa yako kwa bei yenye maslahi kwako.
Kama huna wateja unafunga biashara, na wateja wanapatikana kupitia njia ya masoko. Kwahiyo, ujuzi wa msingi kabisa ambao kila mfanyabiashara lazima awe nao na autumie vizuri ni ujuzi wa Masoko na Mauzo. Siri ya Mafanikio, kwa asilimia kubwa ipo kwenye uwezo wa mfanya biashara kufanya masoko. Masoko yanajumuisha uwezo wako wa kujitangaza na kufahamika. Lazima ujue kuuza la sivo jiandae kuwa sehemu ya takwimu ya biashara zilizofungwa.
Watu wengi hufunga biashara na kusema kuwa sababu kubwa ya wao kufunga biashara ni kwa sababu hawana mtaji wa kutosha, au usimamizi na uendeshaji mbaya, kukosa mda na vitu vingine kama hivyo lakini nyuma ya pazia ni huwa hawana wateja wa kutosha ambao wataingiza mapato ya kufanya biashara ijiendeshe yenyewe.
Unaweza ukawa injinia, au pilot, mwalimu au hata proffessa kabisa tena wa biashara lakini ujuzi wowote ule utakaokuwa nao unaweza usiwe msaada sana kwako kibiashara ukiamua kujiajiri kasoro tasnia moja tu nayo ni ya masoko na mauzo. Lazima uwe na huu ujuzi wa kuuza bidhaa yako kama unataka kufanikiwa kibiashara.
Biashara yoyote utakayoanzisha mafanikio yake yapo katika watu kuifahamu na kuja kupata huduma zako. Biashara ambayo watu hawaifahamu haina maana yoyote. Unaweza kuwa na bidhaa nzuri sana lakini kama watu hawaijui basi lazima utafunga duka. Mfanya biashara ni lazima ujuwe namna ya kutafuta soko, na sio soko ilimradi watu wamekuja lakini soko ambalo umaelichagua wewe, yani unalenga watu wa aina fulani tu ambao watakuja kununua bidhaa yako kwa bei yenye faida kwako, sio ya kuuza kihasara ili mradi umeuza.
Na huo ndio ujuzi namba moja kabisa kwa mtazamo wangu, top of the top skill ambayo kila mfanyabiashara na hata mtu wa kawaida anatakiwa kuwa nao. Lazima ujue kujiuza wewe mwenyewe na lazima ujue kuuza bidhaa zako. Ukijuwa jinsi ya kuuza bidhaa basi unaweza kufanya biashara yoyote tu unayoitaka. Wateja ndio kila kitu katika biashara na hawajileti wenyewe. Lazima uwashawishi, uwe brand.
Njia ya kwanza kabisa nayo ya kufanya masoko, kabla hujakimbilia kujipost mtandaoni ni kuhakikisha biashara yoyote utakayoianzisha, hakikisha ama wewe unakuwa wa kwanza kuianzisha, wa kwanza machoni na kwenye akili za watu au uwe peke yako. Jitofautishe kidogo tu na biashara zilizopo halafu ndio uanzishe biashara yako. Lakini haya tutayaongelea zaidi katika makala nyingine.
Kwa ushauri wa biashara kwa wanaotaka kuanza na mambo kama haya tuwasiliane 0699354779.
Ищите в гугле