1. Soko la Urembo Mchikichini
Soko hili ni muhimu sana kwa wamachinga wote kama vile wale wamasai wanaouza nail cutters, wauza urembo kama vile mikufu, herein na bangili, chupi, leso, vibanio, sox, matoi na vitu vingine vidogo vidogo vya bei rahisi. Hili ni eneo ambalo mtu ukiwa na laki moja tu inakutosha kuanzisha biashara sababu vitu vyake vingi vinauzwa kwa bei ya jumla na kwa bei rahisi.
2. Soko la Ilala
Kama una biashara ya hotel, Genge, catering, muuza nazi, ndizi au mnunuzi wa nazi basi soko la Ilala linakuhusu. Hawa waheshimiwa wanamahali maalum kabisa kwa ajili ya kuuzia nazi kwa bei ya jumla, kuna eneo kwa ajili ya kuuzia ndizi za kula zilizoiva na vitu kama hivyo bila kusahau bidhaa nyingine zote za magengeni. Hapa ndio pa kuzipata kwa bei rahisi. Mkulima ukinunuaukivuna na hujui wapi pa kupeleka mazao yako peleka soko la ilala. Kama unataka kufanya biashara ya mazao pia pitia pale ukajifunze kitu.
Sasa usije ukaenda katika lile soko dogo lililopo machinga complex upande wa Ilala ukadhani hilo ndio soko la Ilala. Soko la Ilala lipo baada ya kuvuka mataa ya Karume kama unaenda Ilala mkono wa kushoto kwa mbele utaona mitumba na nguo nguo nyingi lakini nyuma ya hiyo mitumba sasa ndio kuna soko lenyewe. Vaa Gumbuti kama ni msimu wa mvua.
3. Soko la Mabibo
Kama wewe ni muuza chips basi fanya ziara ya kustukiza katika soko la mabibo ununue viazi moja kwa moja kutoka katika lori. Yani gunia la viazi linatoka katika Lori linaingia kwenye usafiri wako moja kwa moja. Mabibo pia haipo nyuma kwa nazi, ndizi, vitunguu, matikiti na nyanya vyote kwa bei ya jumla. Kama upo mikoani ni mkulima na unauza bidhaa hizi basi fuso lililojaa mazao nenda nalo soko la mabibo uwakabidhi madalali wakufanyie kazi.
4. Soko la Tandika
Soko la Tandika ni maarufu kwa vitambaa lakini bado pia ni maarufu kwa mchele. Ukienda pale sio tu utakuta kuna malori ya mchele yanashusha bali kuna ma semi trailer yanashusha. Pembeni kidogo ya soko la Tandika kuna mafundi wengi sana wa mabegi al maarufu kama vinainai na kwa mara nyingine tena nirudie, vitambaa. Ukihitaji vitambaa nchi hii kuna maeneo matatu tu ya kuvipata napo, kwanza ni Kariakoo Mtaa wa Narun’gombe na Msimbazi, Pili ni Soko hili kla Tandika na tatu, ni Manzese Argentina, nazani ulikuwa hujui hili kuwa Manzese kwa Vitambaa nao wako vizuri Tandika pia kuna mitumba ingawa sio kwa nguvu sana kama….
5. Soko la Karume
Kuna watu wanaishi mjini kwa kuuza mitumba, yani wananunua mitumba soko la Karume, waitoa “sopsop’ wanapiga picha na ku post status na kuuza. Asikwambie mtu kuna mitumba mizuri sana kuliko hata orginal za maduka makubwa na ma mall na ni zaidi ya nguo mpya za Kariakoo za kichina. Soko la Karume ndio madhabahu ya wauza mitumba nchi hii. Hapo ndio ma “baloo” yanapofunguliwa sa 9 usiku usiku. Kwa hiyo kama una ndoto za kuuza mitumba ya nguo, viatu, mikoba basi wakati wa swalaa asubuhi watu wakienda kuswali wewe inabidi uwahi sokoni Karume. Kuna bei ya kila mtu…hela yako tu. Hata 20,000 inatosha kuwa mtaji kama una smart phone na bando la kupost status.
Поиск в гугле