Zifuatazo ni aina 10 za biashara ndogondogo kabisa unazoweza kuzungushia watu chumba kwa chumba kama ni mwanafunzi, nyumba kwa nyumba kama upo mtaani na huna mtaji, na hata kama una mtaji wa fkuwa na meza mahali, frame kama umejichanga au duka kubwa kwenye mall kama umejipanga.
Pipi na Chocolate
Tafuta elfu 10 na nenda Mitaa ya Kisutu, ipo juu ya Mnazi Mmoja kama unaenda posta. Tafuta makutano ya Mitaa ya Aggrey na Kisutu mitaa hiyo imejaa maduka ya za pipi za kila aina duniani humu ambazo zinauzwa kwa bei ya jumla.
Ukiondoa pipi Vitu vidogo vidogo vyote kama vile, biscuit, chocolate na kadhalika vinapatikana mitaa hii kwa jumla. Zunguka zunguka mitaa hiyo kwanza kufanya Scanning kabla ya kuamua wapi pa kununua.
Kuna pipi nzuri sana kifuko kizima cha pipi 200 unakinunua kwa shiling1 4000 tu. Kwa hiyo ukiuza pipi moja Shilingi 100 unapata shilingi 20,000 na kama ukiuza 200/- faida ni kubwa sana. Kama unajua kuuza lakini. Nunua hizi na uzia watoto shuleni, wanafunzi wenzio, stand za mabasi, na kadhalika.
Nguo Za Mitumba
Soko la Karume lipo pembezoni mwa barabara ya uhuru kama unaenda ilala. Linatazamana na Uwanja wa Karume kwa upande mmoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Upande Mwingine. Haya ndio makao makuu ya mitumba Tanzania. Hapo pia nenda na laki tu wala huhitaji mtaji mkubwa sana na uwachagulie wadau nguo nzuri za kuwauzia door to door. Mitumba ya Nguo za ndani, mikoba, viatu, nguo, ma jeans na kila aina ya mavazi inapatikana hapa. Post Status, facebook na Instagram, kwenye ma grupu ya familia, shule na kadhalika na utakuwa tayari kuanza kutengeneza hela.
Nguo Za Ndani
Boxers, Chupi za wadada, tight, vigodoro, Bra, Sidiria na kila kitu chenye sifa ya nguo ya ndani mpya kabisa ambazo utaweza kuuza door to door kutokea nyumbani, mtandaoni, kwenye meza sokoni, stand au popote palopo bize. Makadirio ya Mtaji wa kuanzia ni laki itakutosha kwa kuanzia. Off Course kwa hiyo laki zipo bra tu ambazo brah moja tu inauzwa hiyo laki lakini pia kwa hiyo laki unaweza kupata brah 20 kwani zipo brah unaweza kununua kuanzia hata chini ya 5,000/-. Zipo chupi za wadada unaweza kununua kwa dazeni kati ya 8,000/ – mpaka 13,000 hapo bei ya jumla. Zipo za watoto dazeni (Chupi 12) shilingi 5,000/-.
Urembo wa Nywele,
Kama utataka kusuka wenzio au hata kama wao wanasukana na wanahitaji Nywele zile za extension au rasta na ma wigi na vitu kama hivyo Nenda barabara ya Jangwani inapokutana na Mafia. Mitaa hiyo kuna kila aina ya nywele kwa bei ya jumla. Utahitaji kuwa na zaidi ya laki kwenye mchongo huu. Ukinunua kiwandani moja kwa moja watakudai “deposit” ya milioni 5 lakini ukienda Barabara ya jangwani pale inapoanzia au inapokutana na Msimbazi na unashuka nay a Jangwani kama unaenda klabu ya Yanga…utapata za kununua kulingana na uwezo wako.
Vipodozi;- Mafuta, Perfumes, Sprays, Rangi za Kucha n.k
Mitaa hii hii ya nywele ya Mafia na Jangwani ina maduka ya jumla ya perfumes, lotions, mafuta, sprays aina zote za vipodozi. Kwa hiyo kama ukiamua kuwa sole supplier wa vipodozi kwenye hostel au unataka kuanzisha duka la vipodozi basi nenda mitaa hii. Uwe na hata laki 2 kuanzia na chagua vipodozi ambavyo ni affordable kwa wanafunzi wenzio.
Viatu na Sandals
Kama unaona kuna fursa ya kuuza viatu na vi sandals kwa ajiri ya jinsia ke a jinsia me nenda maeneo ya Mtaa wa Narung’ombe na Msimbazi. Nenda kituo cha mwendo kasi cha Msimbazi kilicho jirani na polisi na utafute Mtaa wa Narung’ombe. Ukishaupata ukipandisha nao kama unaenda soko kuu utakuta machinga wameziba barabara wanauza viatu vya kila aina. Sasa nyuma yao ndio kuna maduka ya jumla ya viatu kuanzia hata buku 3 ila kunakuwa na minimum order kama vile kuanzia pea 12 au 36 za rangi na namba tofauti. sinunue kwa wamachinga. Nenda madukani nyuma yao. Maduka ya jumla viatu vya mbele wanaweka sample tu na hawauzi rejareja. Ukiona unauziwa kuanzia pea moja jua hapo sio. Duka la jumla watakambia wanaanzia dazeni au pea kadhaa, hawauzi moja moja.
Ukihitaji sandals zaidi vuka upande wa pili wa barabara ya Msimbazi, ukiwa na mtaa huo huo wa Narung’ombe..utakutana na maduka ya jumla ya vitambaa, unayapita, ukiwa unabana kulia mwa barabara utaanza kukutana na maduka ya jumla ya vi sandals mengi sana, lakini yapo kwenye vikorido vya ndani ndani. Inabidi uangali angalie kuyaona.
Sandals za Kimasai
Kwa Sandals za kimasai nenda Machinga Complex, Ground Floor. Ukitembea tembea hapo utakutana na vijana wengi sana wanashona viatu vya kimasai. Nunua ukauzie wanafunzi wenzio.
Pochi
Zipo pochi maalum kwa ajili ya mabinti wadogo wadogo, zinaitwa vinainai…zinauzwa zaidi Tandika soko la pochi, bei yake ya jumla vinaanzia 2,500 au 3,000 na kuendelea, mtaani reja reja zinauzwa kuanzia shilingi 5,000/-. Lakini unaweza kupata pochi za kikubwa za ukweli kuanzia soko la Urembo la Mchikichini kule ipo mikoba ya kiwango cha kati ambapo unaweza kupata kati ya 7,000/- na 10,000/- na ukaenda kuuza kwa bei yako. Maeneo mengine bei zake ni zile kubwa kubwa mfano mitaa ya Narung’ombe na Nyamwezi kuna maduka lakini bei zake kubwa . Zaidi ya shilingi 20,000 kwa pochi na sisi tunajadili mitaji midogo.
Flana na Nguo
Vijana wengi wanapenda kuvaa ma jeans na fulana. Kuna mahali fulana ya Form six unaweza kuinunua kuanzia Tsh 4,500 kwa bei ya jumla maeneo ya mitaa ya Aggrey, Mchikichi na mitaa ya maduka ya jirani hapo. Pia ma jeans, mashati na nakadhalika na mambo yote ya nguonguo mpya ni maeneo hayo ya aggrey, mchikichi, kuvuka congo unapandisha kuelekea mitaa ya Sikukuu. Maduka ya jumla wengi watakuambia wanaanzia nguo 3 na kuendelea, fulana hizi mtaani ndio zile tunazonunua kuanzia shilingi 15,000 na kuendelea. Ukiwa na mtaji wa 100,000/- unaweza kuawa na fulana zaidi ya 20 za kuanzia maisha kama mjasiriamali. Usinunue kwa wamachinga au maduka yaliyo barabarani. Ingia ndani ndani kwenye frame za ndani.
Urembo
Hapa tunaongelea kuuza mikufu, bangili, pete, herein, bangles na kadhalika za dhahabu..feki. au za almasi..feki kwani ni chupa tu zimechongwa vizuri. Hivi vitu ni bei rahisi sana ukiwa na laki 3 mpaka 6 zinatosha. Nenda soko la Urembo la Mchikichi lililopo Livingstone na Mchikichi. Maeneo hayo na utachoka mwenyewe
Поиск в гугле