Mawazo 10 ya Kiujumla

  1. Kuwa “Land Lord”

“Wabebe” wanafunzi wengine kwenye chumba chako bwenini. Off course wanakuja na magodoro yao. Tafuta mtu mmoja au wawili “wabebe” na wakulipe kila mwezi. Pesa utakayoipata hapo ni “passive’. Na utaitumia kulipia kodi au”kuwekeza zaidi. Usikae ki boss boss.

Una Kipaji Gani?

Labda unajua kuimba, sio lazima upate “record deal”. Jiimbie mwenyewe ujipost mtandaoni na hata you tube, kuna hela huko,  unajua kucheza mpira au kupiga dana dana kwa kichwa na mgongo..jipost.., unajua kuchora? content hizo..post…, ku fanya gardening..tafuta nyumba chafu rekodi kazi yako…content, kupigana ngumi, karate etc..content hizo maana yake hela. Zama za sasa kuna njia moja tu ya kutajirika chap chap..nayo ni kuwa maarufu. na umaarufu unapatikakana katika mitandao ya kijamii……kwa hiyo kama una kipaji chochote hata kama ni kuongea tu, kuchekesha, kulia kama fisi, kupika pilau nakadhalika wewe kitumie, utapata umaarufu halafu pesa zitakuja zenyewe.

Loan Shark

Kuwa bahili, usimalize boom lako, wenzio wakiishiwa unawakopesha…Mtu akija kukopa unamwmbia weka simu yako, au TV au fridge yako hapo kwanza, ukishamaliza kulipa fedha na riba kwa wakati utachukua vifaa vyako, na ukichelewesha zaidi na deni likawa kubwa na muda wa kulipa kupita vifaa vinauzwa kufidia na..off course, utasaini hapa na hapa na hapa kama mkataba wa mkopo huu, ikibidi acha na nakala ya kitambulisho…hata picha pia sio mbaya. Nothing personal, its Business.Kuwa Kiongozi Serikali Ya Wanafunzi

Hawa jamaa wanaendaga mpaka ulaya, ziara za kujifunza, vikao vya posho vingine na utawala wa chuo, kuna deal za kuo organize events nakadhalika..pia kuna fursa ya kubaki kuajiriwa chuo ukiwa chawa mzuri, kuna fursa za madaraka uki sapoti chama vizuri ..unaweza hata kuwa raisi wan chi siku moja. Uchaguzi ujao chukua form.

Shuguli Shughuli

Kama wewe ni mtu wa matukio na unapenda shughuli shughuli basi ifuatayo ni list ndogo na fupi sana ya shughuli unazoweza kuziratibu na kujiingizia kipato:-

  1. Orientation Week kukaribisha mwaka wa kwanza katika level ya Chuo, Faculty au Bweni. Hii ni shughuli ya kuwaonyesha mwaka wa kwanza mitaa kama vile library hii hapa, ukiumwa hospitali ile pale, bweni la wanawake lile pale, mda wa msosi ukifika Dinning Hall lile pale, ikitokea una somo la sociology, DS, economics na hata political science main hall ndio huwa madarasa ya masomo hayo na hili hapa, ukiibiwa simu kituo cha police kile pale, etc etc
  2. Freshers Ball nayo kukaribisha mwaka wa kwanza ambayo kimsingi ni kuomba ukumbi  kwa Dean of Students na kukodisha DJ apige mziki na mnaweka kiingilio pia katika level ya kichuo au ki bweni au faculty au hata department. Sio lazima uwe ukumbi, hata nje kwenye garden au barabarani kabisa. Weka kiingilio au Uza Soda, Sambusa na kuku.
  3. Concerts ambao kimsingi mnaleta wanamuziki maarufu wanatumbuiza wanafunzi kwa kiingilio. Watu wakipokea boom tu unawaletea wasanii haraka sana kabla hawajanunua vitabu. Wanalipia
  4. Shughuli za Dini ambapo unawaita maaskofu, wachungaji, manabii, walimu, makuhani etc etc  wanakuja kutoa neno kwa wanafunzi..watu waje na sadaka.
  5. Career day ambapo mnaalika makampuni makubwa kwa madogo na waajiri kwa ujumla wakutane na wanafunzi kwa ajili ya internship na fursa za ajira. Unayauzia makampuni nafasi. Unawatoza hela ya ushiriki, ya hema, kiti na meza. Shirikisha uongozi wa chuo. Anzia kwa Dean wa Chuo.
  6. Mihadhara ya Kisomi kwa kuandaa mhadhara ambapo watoa maada maarufu watakuja kuongea na wanafunzi, itabidi kutafuta wadhamini wa nje lkn hata kutoza kiingilio. Waambia watu ITV watakuwepo.
  7. Mihadhara ya Kisiasa na kijamii kama vile ya mazingira, sayansi, teknolojia na kadhalika. Mnaweza kualika taasisi na vyombo vya habari pamoja na exhibitors ambao watalipia.
  8. Fashion shows
  9. Miss Chuo
  10. Shughuli za kujitolea
  11. Marathoni
  12.  Sinema
  13. Tours mfano manenda Nairobi, Zanzibar, Bagamoyo, Comoro etc etc

Kusuka

Ukijua kuosha nywele vizuri tena kwa shampoo, pamoja na kusuka vizuri basi swala la kudanga ukiwa Chuo sahau kabisa. Mambo ya kutafuta Sugar daddy au kujiweka karibu na Mwalimu yatakuwa ni kwa hiari na upendo zaidi na sio lazima.

Kunyoa

Mitaani kuna saluni za kibabe sana. Na kuna wadada wa scrab pia matata sana kukuosha ukimaliza kunyoa…na sometime unapewa massage pia halafu baada ya hapo malipo ni kuanzia 10,000 na kuendelea. Lakini hapo hapo hostel pia kuna saluni…bei yake ni poa pia lakini hamna wadada wa scrab. Kuwepo kwa saluni Hostel hakukuzuii wewe kuwanyoa “washklaji’ kwa gharama kidogo bwenini kwako huku mkipiga story na kucheki movie. 

Make Up Artist

Kuwa mwanafunzi wa kike hakumzuii mwanafunzi kujipost instagram au facebook akiwa anawaka, au kuhudhuria function kama vile birthday yake akiwa anapendeza, kuingia darasani akiwa kapendeza, au kuhudhuria date na public admirer, kuhudhuria harusi za ndugu, jamaa na marafiki, kudanga na kadhalika vyote vinahitaji kupendeza. Wapodoe.

Video Games

    Kila mwenye boom huwaza kununua TV kama mojawapo ya vipaumbele vikubwa sana. Nunua na ile playstation utoze watu kucheza game kama za mpira na kadhalika…chumbani kwako.

    Movies

      Siku hizi mwanafunzi wa chuo kuwa na laptop sio luxury tena. Ni lazima. Nunua Laptop au Desk top yenye graphic card na Memory kubwa tu. Nunua na “external kadhaa, kama 2 hivi za kuanzia na SSD kadi ikibidi. Nenda kwa muuza movie mtaani mwambie akujazie nyimbo, sinema, seriese za kikorea, kihindi na kila kitu…Laki unusu inatosha kama mtaji..wauzie watu kutokea chumbani kwako, ukiwa lecture, library, kitandani etc

      Ku Type na Ku Print

        Ivi unajua kuwa siku hizi hamna kitu kama printer tupu. Pale karikoo mtaa wa kipata na uhuru kuanzia hata 90,000 unaweza kupata ka mashine kana photocopy mashine, kana print na kana scan. Ni kadogo lakini kanafanya kila kitu. Sasa wewe nunua ka kubwakubwa kidogo hat aka laki 2 au zaidi, kaunganishe na kompyuta yako na upo tayari kuanza kutengeneza pesa. Wino ukiisha nenda magomeni mapipa wanauza wini wa kujaza, karatasi nenda kipata ukanunue za dazeni kwa bei ya jumla.

        Trips

          Mfano organize trips za kwenda:-

          1. Zanzibar,
          2. Coco Beach
          3. Jangwani Beach
          4. Kigamboni,
          5. Ngorongoro,
          6. Mikumi,
          7. Mlima Kilimanjaro
          8. Udzungwa
          9. Nairobi

          Na kwingineko.

          Kuajiriwa (Part Time Jobs) na Internship

          1. Gym Trainer/Bouncer, kila chuo kina gym 
          2. Network Marketing..waone Forever living, Oliflame, nafasi hazijaagi
          3. Kuwa MC “ Msema Chochote”..anza kama chawa wa MC kwanza
          4. Kuwa Influencer:- Post sana uzushi wowote tu
          5. Website Designing kama hujui tutafutane 0699 354779
          6. Graphic Designing kama hujui tutafutane 0699 354779
          7. Video Editing kama hujui tutafutane 0699 354779
          8. Social Media
          9. Ijue ChatGPTkama hujui tutafutane
          10. Tutor
          11. Blogging kama hujui tutafutane
          12. Membership Site kama hujui tutafutane
          13. Classified Ads Website kama hujui tutafutane
          14. Udalali

          Vitu Vya kutengeneza Na Kuuza

          • Keki na kama hujui tutafutane 0699 354779
          • Vi tafunwa na kama hujui tutafutane 0699 354779
          • Sabuni na kama hujui tutafutane 0699 354779
          • Lambalamba na kama hujui tutafutane 0699 354779
          • Karanga na kama hujui tutafutane 0699 354779
          • Chakula kama hujui mcheki mama ntilie aliye jirani yako

          Uza Bidhaa

          Kama hujui pa kuanzia tutafutane 0699 354779 kwa ushauri

          • Nguo
          • Nguo za Watoto
          • Nguo za Ndani
          • Viatu
          • Vipodozi
          • Urembo
          • Pipi

          Ukitaka kujifunza kwa gaharama nafuu, biashara yoyote kati ya zilizoainishwa hapa, tuwasiliane 0699 354779

          1 Comment

          Leave a Reply

          Your email address will not be published. Required fields are marked *