Mojawapo ya biashara za muda za GIF ilikuwa ni kiwanda kidogo cha kutengeneza mikoba inayo match na Sandals au viatu vyake kwa maana ya flat shoes. Lebo yetu tuliita Gabriella. Na Kabla ya Hapo tulianza kushona Ma Jeans tu. Malighafi ya vyote hivyo hapo awali tulianza kununua kutoka Dubai kwa maana ya vitambaa lakini pia Mashine zote za viatu tulitoa China. Kwahiyo, hapa GIF tulianza kwenda China kibiashara tokea miaka hiyo ambayo sio kila mtu alikuwa anaweza kuamka na kwenda kama ilivyo sasa na mpaka leo hii bado tunaenda mara kwa mara kwahiyo tuna experirnce nzuri na namna mizigo inavyonunuliwa na kutumwa kutokea China.

Sasa hivi kuna wimbi kubwa sana la watu wanaenda China na wakiwa huko hufanya promo, hujipost mtandaoni kutafuta watu wa wanaotaka bidhaa kutoka China wawatumie hela ili waweletee. Makala hii itaangalia mambo matano mafupi ya kufahamu kabla hujamuagiza mtu

  1. Unapoambiwa utaupata mzigo ndani ya mwezi ni bora ukafikiria mara mbili. Waafirika wengi wakienda China hununua mizigo yao katika masoko ya Guangzhou katika maeneo yanayoitwa Xiobei na Sunyianil. Huku ndio maeneo yenye maduka mengi sana ya reja reja pamoja na wamachinga wa kichina ambayo kwa bei zao kwetu ni sawa wanauza kwa bei ya jumla. Maduka mengi huwa hayana mzigo mkubwa au wanaita “stock’ na huwa wanaweka sample tu madukani. Kama mtu unahitaji mzigo mkubwa unaweka order kwa hawa wauzaji wadogo wa kichina, nao wanaenda kuweka order kiwandani, halafu unasubiria wiki moja hadi 2 mpaka mzigo uwe tayari, ndio ukauchukue.

Mara nyingi mtu akipost umuagize China maana yake anakuwa China wiki 2 anasubiria order yake ikamilike na muda huo anahitaji kula na kulala hotelini huko na anakuwa hana cha kufanya zaidi ya kuzurura madukani siku nzima. Kwa hiyo ukimuagiza anapata na yeye pesa ya kumuweka huko anasubiria mzigo wake. Changamoto ni kuwa inawezekana mzigo utakamuagiza wewe nao utatakiwa ausubirie wiki 2 nyingine, na mwingine akija hivyo hivyo na yeye tiketi yake ya kurudi tayari ipo confimerd kwa hiyo itabidi akuagizie na awaachie wachina au Wabongo wengi waliopo China wanafanya shughuli hizo za udalali na u guide wa wageni wamtumie mzigo ukiwa tayari. Sasa kama order inachukua siku 10 mpaka 14 kuwa tayari huo mzigo hauwezi kukufikia ndani ya mwezi mmoja.

  • Safari ya meli kutoka China kuja Afrika ni sawasawa na daladala tu. Madaladala mengi hayatoki stand kubwa mpaka yajaze. Na ni hivyo hivyo kwa meli. Meli haiwezi kupakia mzigo wako tu, kibox kimoja na ikaondoka nao. Lazima container lijae, kunaweza kuwa na ma container 1,000. Yote yajae ndio meli iondoke na hayajai kama daladala linavyojaa. Inachukua muda kwa meli kupata mzigo wa kutosha ili iondoke. Tarajia kupokea mzigo wako kuanzia miezi 3 na kuendelea ikibidi mpaka mitano. Utaenda ofisi za wakala, utalalamika, utalia utafanya vurugu zote lakini usitarajie mzigo chini ya miezi mitatu, labda mzigo wako ndio uwe wa mwisho kuingia kwenye container na container lako likipakiwa tu na meli inaondoka.

Unapoambiwa mzigo utafika ndani ya mwezi maana yake amtu anaekuagizia inawezekana nae kadanganywa na watu wa masoko wa kampuni za usafirishaji au wachina wamemdanganya au ana njaa kali sana anahitaji hela kwa namna yoyote ile. Mambo mengine atajua mbele kwa mbele.

  • Hela ya kutumia mzigo hautumi ukiagiza mzigo. Unalipia mzigo wako ukifika dar na ukiwa tayari umetolewa bandarini. Wewe unaenda kuuchukulia store ya kampuni ya usafirishaji uliyoiagiza. Store nyingi zipo maeneo ya viwandani keko kule lakini pia zipo maeneo mengine ya mji. Ukipokea mzigo unakuta kampuni ya usafirishaji imemalizana na TRA, na gharama zote zinazohusiana na usafirishaji mzigo. Unalipia, unabeba, unaondoka. Ukiambiwa lipia na hela ya usafiri kabisa kabla mzigo haujatoka China basi huo mzigo maana yake unakuja kwa ndege.
  • Unaemuagiza mzigo akikupa bei rahisi sana ya bidhaa unayotaka kuagiza maana yake gharama za usafiri hajaweka humo. Mfano unaambiwa TV inch 75 shilingi 300,000/- wakati hiyo TV inauzwa Milioni unusu madukani Dar basi hapo ujue gharama za Usafiri hazijaingizwa na uweke pembeni laki 5 au zaidi za kumpa dalali wako mpaka aje akupokelee hiyo TV. Kama umeagiza na hela yako yote na huna ya kutolea basi unaweza usiupate mzigo wako.
  • Kama umeiona bidhaa unayoitaka Alibaba, ukataka uifate basi jua mara nyingi bei unayoiona Alibaba sio bei ya kuuzia mzigo. Bei zilizopo Alibaba ni za promotion tu. Kwahiyo kama ukiona mashine fulani unayoitaka imeandikwa inauzwa dola 5,000/- mtandaoni Alibaba basi jua hiyo bidhaa bei yake ya ukweli ukienda China inaweza ikawa Dola 10,000 au zaidi. Lakini wachina hawana tabia ya kukataa hela na watakuletea mashine tofauti, ndogo na tofauti na uliyoiagiza, na kama ukisafiri kwenda kuinunua hiyo mashine na mfukoni umebeba hela ulioiona mtandaoni basi jiandae kurudi mikono mitupu….lakini utakuwa umepanda ndege na umenunua raba ukirudi.

Mwisho wa siku ukihitaji kununua bidhaa kutoka China ni bora safari ya kwanza ukaenda wewe mwenyewe, kama ni mtu wa mzigo mkubwa unaenda kiwandani kabisa na uanunua mzigo wa kwanza na kuacha mawasiliano yako na waliokuuzia, baada ya hapo utakuwa unaagiza tu na wachina wanakutumia wao wenyewe. Wachina watu poa sana na sio wabaya kama watu wengi wanavyowadhani.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *