Siku zote kumekuwa na gumzo la watu kuongelea kuwa siku moja wanataka kuanzisha biashara fulani ambayo inahusisha kutoa mzigo fulani Zanzibar na kuuleta bara kwa ajili ya kuuza huku. Kama mfanyabiashara nnaejua mambo kadhaa kuhusiana na bidhaa kutoka Zanzibar naomba nikupe mambo 5 yafuatayo kuhusiana na kuchukua mzigo kutoa Zanzibar
Ukitaka kwenda Zanzibar kuna usafiri wa boti na ndege. Vyovyote vile ni lazima ubebe kitambulisho. Usafiri wa Boti unachukua kama lisaa limoja na nusu kwe meli za Azam au Zanzibar One na nauli ni kuanzia 30,000 wakati wa kuandika makala haya. Kuna meli za kwenda na kutoka Zanzibar sa 1 asubuhi, sa 3, sa 6, sa 8 na sa 10 jioni. Meli za jioni zina mawimbi makali sana.
Unaweza ukaenda na kurudi siku hiyo hiyo.Kama upo dar Unaweza kwenda na gari yako mpaka mjini ukaicha parking ukaenda Zanzibar na ukarudi siku hiyo na kurudi na gari yako.
Mizigo mikubwa au mizito kutoka Zanzibar inakaguliwa Bandarini na kuna malipo ya kufanya kama vile kulipa kodi ingawa ni kodi laini kidogo, hawakukomalii kama vile umetoka ulaya ambapo hata shati moja jipya unaweza ukaambiwe ulilipie kodi.
Zanzibar inajulikana zaidi kwa Utalii na Viungo au spices kama vile karafuu lakini hapa tutajadili bidhaa nyingine na zifuatazo ni bidhaa tano ambazo unaweza kununua Zanzibar na kuja kuuza bara
- Vipodozi:- Maduka mengi ya vipodozi yapo nyuma ya soko la marikiti au stand ya mabasi ya shamba. Ukifika bandaraini chukua boda au bajaj waambie wakupeleke Soko la Darajani, Stand ya mabasi ya shamba. Hapo utakuta kuna jengo moja refu kama treni. Nyuma yake hilo jengo kuna Stone Town. Zile nyumba zenye mitaa myembamba kama vichochoro mitaa hiyo hiyo na mpaka nyuma ya soko la samaki pamaja na soko la marikiti ndio Stone Town kwenyewe na utakuta maduka kadhaa ya vipodozi ambavyo unaweza kuja kuuza bara
- Mafridge Used;- Kama kuna bidhaa imejaa Zanzibar basi moja wapo ni ya fridge used. Hii mitumba ya fridge imezagaa karibu Zanzibar yote. Ukifika Zanzibar litafute eneo linaitwa kwa mchina. Kuna kwa mchina mwanzo na Kwa mchina mwisho lakini barabararani mitaa yote hiyo kuanzia kwa mchina hapo kuna mafridge maeneo mengi sana. Utayaona tu nje. Bai yake haina utofauti sana na bei inayouzwa Magomeni Dar, lakini kule zipo nyingi sana kuliko za Magomeni Mapipa.
- TV Used:- Hapo hapo kwa mchina ndio machimbo yake. Zimejaa hapo. Zipo ambazo zipo tested kwa maana zimejaribiwa na ni za uhakika na zipo ambazo hazija testiwa. Hizi ambazo hajitestiwa bei yake ni rahisi sana unaweza ukakuta TV inch 40 inauzwa laki unusu, lakini inaweza kuwa nzima au mbovu pia.
- Vifaa vya Umeme:-Huno kwenye soko la darajani kuna mahali panaitwa mtendeni au soko la mtendeni. Hapo ndio kuna maduka mengi sana ya vifaa vya umeme vipya kama ma Radio, TV, Pasi, Subwoofer, na vifaa vingine vya umeme. Ukitaka kununua hivi basi ukifika Zanzibar , nenda darajani Souk, na huma kwenye souk, katikati, kuna mahali panaitwa Mtendeni, kuna bidhaa za umeme nyingi sana.
- Baiskeli Used:-Hapo hapo kwa mchina pia ni chimbo la baiskeli used za kila aina used za watoto na za watu wazima. Unaweza kununua kule 60,000 ukaja kuuza dar 120,000/-. Fanya uchunguzi.
- Ubuyu wa Babu Issa:- Babu Issa anauza ubuyu wake ndoo ndogo shilingi 45,000 na kubwa 60,000/-. Ofisi zake zipo Stone Town. Ukifika pale darajani Souk kuna mataa. Hapo kwenye mataa kunja kulia halafu ulizia mitaa hiyohiyo. Wala hayupo mbali.
- Ukihitajikuuza khanga za Zanzibar ni whatsapp 0699354779 nkuelekezi mahali utakapo pata mzigo wa bei ya jumla.
Zanzibar inategemea bidhaa zake nyingi kutoka bara kwahiyo usiratajie kuwe na vitu vingi sana kule. Nguo nyingi ni za kariakoo, vyakula pia vinatoka bara kwahiyo fursa sio nyingi sana. Labda ukatalii.
Поиск в гугле