Watu wa mjini wanamsingizia sana mtoto wa Kikwete. Ridhiwani. Kila wakiona kitu cha gharama utasikia cha Ridhiwani kile, vituo vya mafuta vya Ridhiwani, malori yote nchi hii ya Ridhiwani, kila deal la hela la Ridhiwani lakini ukweli ni kuwa Ridhiwani anasingiziwa. Pamoja na kuwa ana jina la kitajiri lakini hana hela hiyo.
Ukiongelea matajiri wa Tanzania unaongelea akina Mohamed Dewji, akina Bakhresa, GSM kilefu chake Gharib Said Mohamed, Shubash Patel, Ally Awadh, Shubash Patel, Shekar Kanabar, Rostam Aziz, Salim Turkey, Shamim Deo lakini pia walikuwepo marehemu Mengi na Manji kwa kuwataja wachache.
Wengi kwenye hiyo list hutuwafahamu sababu hawana tabia ya kujisnap na mabulungutu ya pesa tik tok. Matajiri wa kweli hawanaga hizo. Wao utawaona wakati wa kutoa misaada baada ya mafuriko au njaa au baada ya mungu kuwapiga tukio kubwa waswahili na serikali kulazimika kupitisha bakuli ili kuwasaidia. Rais akiwaalika ili awapige mzinga na mwisho wakati wa kuagana akipiga nao picha ya pamoja ndio Watu tutabahatika kuwaona wanafananiaje kwa kuwaona gazetini au mtandaoni kesho yake, utasikia..” ivi balesa ndio uyu, na uyu ndio giesiem…..mbona janki sana.
Tajiri pekee ambae watu wengi wanamjua kafananaje ni Mo Dewji sababu jamaa anaandamwa na neema pamoja mabalaa mengi yakiwemo kuandamwa sana na maskini, lakini pia ana trend sana mara utasikia ndio bilionia kijana Afrika, mara utasikia katekwa, na sie mashabiki wa Simba timu ikifungwa lawama kwake…utatuona kwenye comment mtandaoni tunadai Mo amfukuze kocha, avunje mkataba wakati tunajua kuvunja mkataba kuna gharama zake na hatulipi sisi.
Sasa hawa watu hela zao za kila siku wanawekeza wapi na sie tukawekeze ili tuwe kama wao. Tupate mawazo ya biashara hapa kwa kuangalia maeneo matano ya wawekezaji na matajiri makubwa wa Tanzania.
- Hawa waheshimiwa wamewekeza sana katika uzalishaji ukiwemo wa vitu vidogo vidogo hasa vyakula na vinywaji. Kuanzia biskuti, pipi, chapati, ice cream, unga, mikate,pipi, na vitu vya namna hiyo ambavyo wewe unavichukulia poa na kuviona havina maslahi. Wenzio wanakusanya hamsini hamsini na wanakuwa na hela za kutosha kuishi duniani kama mbinguni.
Biashara hizi zinaugumu wake, zinahitaji watu kwa maana ni labor intensive lakini pia zinahitaji mitaji kwa maana ni capital intensive lakini zina wateja wengi wengi sana sababu zinaendana na mahitaji halisi ya Mwafrika. Mwafrika uwezo wake ni kujinunulia chakula kwa hiyo na wewe wekeza humo. Ulaya hawawazi sana mambo ya kula na huwezi kukuta muuza chakula ndio tajiri mkubwa. Huko matajiri wakubwa ni wauza teknolojia, software na Fasheni na vitu kama hivyo.
- Matajiri wengi wakubwa pia wamewekeza kwenye madini. Nchi yetu ina utajiri wa madini kwa hiyo ukihitaji mahali pa kuwekezaili utajirike kawekeze kwenye madini. Sekta ya madini ni pana sana, sio lazima uingie shimoni kusaka dhahabu au Tanzanite unaweza ukawa unauza na kukodisha vifaa kuanzia vya kuchimbia mpaka vya kuyatafuta madini yenyewe yalipojificha au ukawaachia watu wengine wachimbe wewe unanunua kwao na kwenda kuuza uarabuni au unaweza kuwa dalali tu wa kuwaunganisha wachimbaji na wateja wao, au safirisha tu madini kama vile makaa yam awe na kadhalika.
- Mafuta na Nishati: Matajiri kama akina Mo dewji, Ally Awadh, Rostam Aziz wao wamewekeza kwenye sekta ya Nishati na Mafuta Wakati mwingine sio lazima umiliki kisima cha mafuta uarabuni, unaweza kujenga maghala ya kuhifadhia mafuta tu na wanaonunua uarabuni wanakuja kuhifadhia kwako au Jenga vituo vya mafuta kila mtaa, au safirisha tu mafuta, Uza gesi kama ilivyokuwa kwa Manji, iuzie Serikali umeme na hali kadhalika basi na wewe utakuwa tayari kwenye mkondo wa hela.
- Kilimo:- Matajiri wa nchi hii wamewekeza kwenye kilimo hasa kilimo cha mazao ya biashara kama vile katani, chai, korosho, ufuta, tumbaku na vidhaa kama hizo za kimataifa. Kwa hiyo kama unataka kuwa tajiri mkubwa kilimo cha mboga mboga kinaweza kikakupa hela ya kula, lakini kama unataka kuwa tajiri basi wekeza kwenye mazao ya kibiashara, hasa yale utakayoweza kuyachakata na kuza kama bidhaa iliyokamilka. Kwa mfano badala ya kulima na kuuza katani kwanini usitengeneze na kuuza kamba au magunia kabisa.
- Majengo au Kwa Kiingereza Real Estates: Ni tajiri gani asiyewekeza kwenye majengo? Yale maghorofa marefu mjini yanamilikiwa na akina nani kwani? Tunajua siyo ya Serikali na yote sio mali ya taasisi za umma kama NSSF na PSSSF. Kwa hiyo ya nani yale? Jibu ni kuwa ni ya watu binafsi kwa sababu matajiri wote wanawekeza faida wanayoipata kutoka katika biashara zao za awali kwenye majengo.
Kwa mfano Bakhresa anamiliki meli za Azam Marines na kwa siku anaweza kusafirisha abiria 10,000. Kuna siku meli huwa zinajaa zote. Sasa kama kila abiria akimlipa nauli ya 30,000/- . Jibu ni hela nyingi sana kwa siku na anaweza kujenga ka apartment ka moja kila siku.
Sababu hela anazopata ni nyingi inabidi aziwekeze. Majengo ni mkondo mzuri sana wa fedha sababu eneo linalokuingizia hela inaingia ukiwa umelala, zinakufanya uwe na ukwasi sababu zinaingiza hela ndani ya mda mfupi wa kusubiri, lakini unaweza kukopea, unaweza kuuza sababu thamani yake inapanda. Automatikale.…ok kuna gharama kidogo za hapa na pale lakini ni passive income.
Sasa sio lazima ujenge nyumba na kupangisha tu, unaweza kujenga nyumba na kuuza, kama unadhani gharama zake ni kubwa basi wewe nunua viwanja na jenga nyumba lakini usiweke finishingi, unajenga msingi, unanyanyua, unafunika na bati na unakuwa umemaliza, unauza hivyo, au unaweza kununua nyumba chakavu, unazifanyia ripea na kuziuza tena.
Manji, Bakhresa na GSM ni wachache ambao wamewekeza katika majengo ya makazi, ofisi na kadhalika.
Sasa tupige story za kimaskini hapa, Mwaka mmoja una miezi 12, jaribu kuwa na ndoto ya kuwa na apartment 12 kwanza kwenye location nzuri. Maana yake utakuwa unavuta kodi kila mwezi mwaka mzima. Kama wewe ni mpambanaji mzuri au mla rushwa, au jizi uliyebobea jaribu kuwa na nyumba 52, maana yake kila nyumba itakulisha kwa wiki moja, yani kila wiki kuna mpangaji anakulipa kodi ya mwaka, au amua kuwa Baba lao, miliki apartment 370!!hapo una nyumba inakulipa kodi kila siku mwaka mzima, na mameneja wa benki watakuwa wanalala na kuamkia mlangoni kwako, unakuwa umefikia level ya kujenga kwa hela za watu wengine sasa. Hutuimii hata 100 yako .
Ищите в гугле