Kama unapenda urembo, mambo ya u model, u miss, ku design basi biashara hii ya kushona nguo za wanawake itakufaa.

Siku hizi kuna Nguo za wamama zinashon wa ushwahilini halafu zinauzwa kama zinatoka Uturuki na huwezi kujua kama zimeshonwa humuhumu mitaani na ma fundi wa kawaida kabisa.

Biashara hii itakufaa sana kama una akili nzuri ya mambo ya fashoni na mitindo, unajua kuchagua vitambaa na kuchanganya rangi na material na urembo tofauti tofauti.

Kuanzisha biashara hii haimaanishi kuwa uwe unajua kushona wewe mwenyewe lakini inamaanisha kuwa uwe unajua kuisimamia ili kuhakikisha ubora na mitindo inabaki kuwa ya hali ya juu, mambo ya kushona wapo mafundi wengi ambao utawatumia kama dei waka,

Lakini vile vile unaweza hata usiwe na cherehani hata moja bali unakuwa na duka tu kwani unatafuta mafundi wako wazuri watakaokuelewa unahitaji nini, wanakushonea na wewe unakwenda kuuza, ingawa utahitaji kuwa fundi mmoja karibu kwa ajili ya kufanya marekibisho madogo madogo ya kupunguza na kuongeza size kulingana na matakwa ya mteja.

Angalizo, mwandishi wa makala haya aliwahi kushona nguo pia za wadada, actually bado anashona hizi nguo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *