Siku hizi kuna mafundi wa kushona nguo wanaopanga frame ya kulipa zaidi ya laki 5 kwa mwezi, kwa hiyo kama bado una mawa- zo kuwa fundi cherehani ni mtu flani ane- shonea kibarazani ili kupata hela ya kujik- imu tu basi umepitwa na wakati.
Kama unadhani pia kuwa fundi wa nguo mpaka wewe mwenyewe ndio ujue kusho- na na kupima watu pia umepitwa na waka- ti. Siku hizi tasnia ya kushona nguo ime- badilika na nguo ya kushona imekuwa ya heshima na gharama zaidi kuliko hata ya kununua dukani.
Unaweza kuanzisha biashara ya kushona kwa ku specialize, mfano unaweza kufun- gua karakana ya kushona suti za wanau- me tu basi, umemaliza. Zinaweza kuwa ni suti za Ofisini, Suti za Maonyesho, suti za harusi na kadhalika.
Unaweza kushona nguo za kiume kama za Ki Nigeria tu kwa maana unachanganya vitenge pamoja na ku darizi na vitu kama hivyo.
Mtaji wake sio wa kutisha sana kwani uta- hitaji cherehani kadhaa industrial, utahita- ji mashine ya Overlock, utahitaji pasi, uta- hitaji meza, vitambaa na mahitaji mengine madogo madogo na upo tayari kuanza.
Angalizo, mwandishi wa kitabu hiki aliwa- hi kumiliki kiwanda cha kushona jeans, vitambaa alinunua deira, dubai.
Поиск в гугле